Soka saa 24!

Rasmi Manchester City yamsajili, Riyad Mahrez 

Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City wamethibitisha kumsajili mchezaji, Riyad Mahrez kwa dau la pauni milioni 60 kutokea Leicester City.

Mahrez ambaye amesajiliwa kwa dau lililoweka rekodi ya klabu hiyo marakadhaa amekuwa akitakiwa na City lakini dili likigonga mwamba.

Miamba hiyo ya soka ya Uingereza imekamilisha kandarasi ya winga huyo wa Leicester ambaye amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 13 kwenye michezo yake 41 aliyocheza akiwa na mbweha hao msimu uliyopita.

Winga huyo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Manchester City na kufuta rekodi iliyowekwa na beki wa Ufaransa, Aymeric Laporte aliyetua hapo kwa pauni milioni 57 mwezi Januari.

Mahrez alijiunga na Leicester mwezi Januari mwaka 2014 na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Sky Bet Championship.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW