Habari

RASMI: Mtangazaji wa EFM Maulid Kitenge ahamia Wasafi FM, Atoka na wenzake wawili na kumvuta Eddo Kumwembe (+Video)

Mtangazaji maarufu wa Habari za Michezo nchini Tanzania, Maulid Kitenge ametangaza rasmi kuwa ameachana na Kituo cha Redio cha EFM alichokuwa anafanyia kazi na kujiunga Wasafi FM, Radio  inayomilikiwa na mwanamuziki, Diamond Platinumz.

 

Akithibitisha kuondoka kwake EFM kwenye mahojiano na Bongo5, Kitenge amesema kuwa ameondoka rasmi kituoni hapo Juzi jumanne na ameondoka kwa kheri kabisa bila shari.

Maulid Kitenge alikuwa mtangazaji wa E-FM tangu mwaka 2015 akiwa kama Mkuu wa Idara ya Vipindi vya Michezo, huku akitangaza vipindi vya michezo vya Sports Headquarters na E-Sport, pamoja na kusoma magazeti kwenye Kipindi cha Joto la Asubuhi ndani ya EFM iliyoko Kawe Beach Jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa E-FM wamemtambulisha msanii, Elizabeth Michael ‘Lulu’  kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi kama mbadala wa Kitenge.
Kitenge amejiunga rasmi na Wasafi FM ambapo atakuwa akiongoza Kipindi cha Michezo cha Sports Arena na atakuwa na mchambuzi mkubwa wa michezo Tanzania, Edo Kumwembe.
Wengine walioondoka na Kitenge, Ni Yusuph Mkule na Mwanaidi Suleiman ambao wote alikuwa anafanya nao kazi.
Ni kweli nimeachana na EFM na nimehamia Wasafi FM ambapo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo nitakuwa nafanya Kipindi cha Sports Arena ambacho kitakuwa hewani kuanzia saa mbili hadi saa tano asubuhi, lakini pia nitakuwa nasoma magazeti kwenye kipindi cha asubuhi saa moja na nusu. Katika kipindi hicho nitakuwa na Yusuph Mkule na Mwanaidi Suleiman ambao nilikuwa nikifanya nao kazi EFM, pia nitakuwa na watangazaji wengine kama Edo Kumwembe na Ahmed Abdallah,” amesema Maulid Kitenge.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents