Burudani ya Michezo Live

RASMI SASA : Kakolanya atua Simba SC, mabingwa hao wa TPL wamvulia kofia “Hakuna ubishi huyu ni moja ya makipa wenye uwezo mkubwa nchini”

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba SC hii leo wamemsajili aliyekuwa mlindalango namba moja wa wa hasimu wao Yanga SC, Beno Kakolanya kwa kandarasi ya miaka miwili.

Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram, Simba imeweka hadharani picha aambazo zikionyesha nyota huyo akisaini mkataba na miamba hiyo ya soka yenye maskani yake mitaa ya KariaKoo.

“Ni Beno Kakolanya. Hakuna ubishi kuwa huyu ni moja ya makipa wenye uwezo mkubwa nchini na tunaamini akishirikiana na wenzake katika kikosi chetu watatuwezesha kuongeza ukubwa wa timu na kutupatia mataji msimu ujao. Tumeshamalizana nae kwa mkataba wa miaka miwili.”- imeandika akaunti hiyo ya instagram ya Simba.

Kakolanya aliondoka ndani ya Yanga mara baada ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kumtaka atafute timu nyingine kutokana na mlindalango huyo huyo kugoma kwa siku kadhaa kuichezea timu yao akiwa anashinikiza alipwe madeni yake ya pesa za usajili.
Iliwahi kuelezwa kuwa Kakolanya alikuwa akiidai Yanga Tsh Milioni 15 za usajili lakini baada ya mdau wa Yanga kumpa kiasi cha pesa cha Tsh Milioni 2 alitaka kurudo aendelee kuichezea timu hiyo lakini kocha wake Mwinyi Zahera akamkataa na kusema hamuhitaji tena mchezaji huyo kutokana na kugoma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW