Michezo

RASMI: Simba SC wamtangaza kocha mpya, Soma CV yake

Klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi Mfaransa Pierre Lechantre, kuwa Kocha mpya atakayekinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa hakina mwalimu baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog mwishoni mwa mwaka jana.

Pierre Lechantre

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na Mfaransa huyo atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida United leo Januari 18, 2018 katika Uwanja wa Taifa.

Mfaransa huyo alishawahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.

Soma zaidi taarifa hiyo kutoka Simba SC;

                                          TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroon kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.
IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA SC NGUVU MOJA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents