Habari

Ratiba ya kuuaga mwili wa kiongozi wa CHADEMA yatangazwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kinatarajia kuongoza shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Hananasif, Jimbo la Kinondoni, Daniel John siku ya kesho Jumanne Februari 20, 2018.

Tokeo la picha la Chadema Mbowe auawa
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe akionesha picha ya marehemu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene imeeleza kuwa mwili wa marehemu Daniel unatarajiwa kufika nyumbani kwake Hananasif, ukitokea hospitali ya Taifa Muhimbili majira ya saa 4 asubuhi na kisha kupelekwa katika Kanisa la Katoliki la Kwa Pinda kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu itakayoanza saa 5 asubuhi kanisani hapo.

Baadaye, waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho kwa Daniel kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa siku ya Jumatano, katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.

Soma taarifa hiyo zaidi;


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents