Michezo

Ratiba yaibeba Yanga SC Kombe la Mapinduzi, Simba kundi la kifo

Wakati mashindano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar yakitarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi tarehe 30 ya mwezi Desemba, ratiba ya michuano hiyo imetoka ambayo inajumuisha jumla ya timu 10 zitakazoshiriki ambazo zimegawanywa katika makundi mawili ya A na B.

Katika michuano hiyo Klabu ya Yanga ambayo ipo katika kundi B, ipo pamoja na timu za Zimamoto, Mlandege, Shaba na JKU. Kutokana na timu zilizopo katika kundi B, wadau wasoka wanaona kuwa Yanga SC ratiba hiyo inaibeba klabu hiyo hasa kutokana na uwezo uliyokuwa nayo ukilinganisha na hizo nyingine.

Katika kundi A, kunatimu za Simba SC, Azam FC, URA, Jamhuri na Taifa Jang’ombe. Kutokana na timu zilizopo katika kundi hili basi huonyesha wazi ugumu uliyopo.

Yanga SC itashuka dimbani Januari 1 mwaka 2018 katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya JKU kisha kuikabili  timu ya Shaba Januari 3 katika mchezo wake wa pili wa kundi hilo.

 

Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Yanga SC, George Lwandamina ametoa siku saba za mapumziko kwa wachezaji wake na wakitaraji kurejea tena jumatatu ijayo tayari kwa maandalizi ya duru ya 12 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents