Burudani ya Michezo Live

Raul Jimenez, Jadon Sancho safari imeiva Man United, Bale aiganda Madrid kama ruba

Uhamisho unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo, 20. (Independent)

Sancho alijiunga na Dortumund akitokea Manchester City mwezi Agosti mwaka 2017

Mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, yuko njiani kuelekea Manchester United baada ya Wolves kukubali ada ya pauni milioni 27 kumsajili mshambuliaji wa Braga, Mreno Paulinho. (RTP,Express)

Chelsea imeweka mezani ofa kwa ajili ya mlinda mlango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 28. (Cadena Ser, via Mail)Raul Jimenez kwenda Manchester United

Gareth Bale, 31, amemwambia kocha wa Wales Ryan Giggs kuwa ana dhamira ya kusalia Real Madrid msimu ujao. hata kama kukosa michezo kutaathiri kipato chake. (Mirror)

Gareth Bale kusalia Real Madrid hata kama mshahara wake utakuwa na sintofahamu

Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza katika kumfuatilia mchezaji David Alaba, 28, ambaye huwenda akasaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Telegraph)

Leeds wanapanga kusajili wachezaji wawili- Kiungo wa Everton Fabian Delph, 30, na beki Danny Rose,30, wakati huu ambapo kocha Marcelo Bielsa akitafuta wachezaji wenye uzoefu na ligi ya primia. (Star)

Mlinda mlango Muajentina Sergio Romero,33, anataka kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu mustakabali wake- huku Dean Hanserson,23, akirejea Old Trafford baada ya kukipiga kwa mkopo Sheffield United (Sun)

Inter Milan wanatarajiwa kukubali dili kumsajili Mshambuliaji Alexis Sanchez,31 kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu msimu huu. (Manchester Evening News)

Southampton bado wanaisubiri Tottenham kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Pierre-Emile Hojbjerg ,24. (Daily Echo)Mesut Ozil

Kiungo wa kati Mesut Ozil, 31 atasalia Arsenal msimu huu. (Mail)

Liverpool wanajiandaa kumsajili mchezaji wa Bournemouth Lloyd Kelly, 21, baada ya kupoteza fursa hiyo miezi 12 iliyopita alipokuwa akiichezea timu ya Bristol City. (Express)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp pia atafanya maamuzi kuhusu mshambuliaji wa Kiingereza Rhian Brewster,20, baada ya mchakato wa kucheza kwa mkopo Swansea kufanikiwa. (Liverpool Echo)David Alaba (katikati) ameisaidia Bayern Munich kunyakua mataji manne ya Bundesliga

West Ham United wana mpango na mchezaji wa Queens Park Rangers, Ryan Manning, 24. (Telegraph)

Atletico Madrid imekataa ofa ya pauni milioni 22.6, na kiungo wa kati Matteo Guendouzi, kutoka Arsenal kwa ajili ya kiungo wa kati Thomas Partey, 27 (AS in Spanish)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW