Habari

Ray akionesha kifaa kilichoifanya kampuni yake kuchukua tuzo ya ‘Best Production Company’

Muigizaji, muongozaji na mtayarishaji wa filamu nchini Vincent Kigosi aka Ray, ameionesha camera yake ya ‘maangamizi’ ambayo anasema ndio siri ya kampuni yake (RJ Company) kushinda tuzo ya kampuni bora ya utayarishaji wa filamu nchini kwenye tuzo za Steps Entertainment 2013 wiki iliyopita.

6f215584d81a11e2a13a22000aaa05ca_7

“Hii ndio siri ya RJ Comapany kuwa best production company 2013 kwenye tuzo za Steps Awards,” ameandika Ray kwenye picha ya camera hiyo aliyoiweka kwenye Instagram.

a5bb3470d81a11e2867a22000a9f1266_7
Camera hiyo imevuta attention ya muongozaji wa video za muziki nchini aliyetokea kupata umaarufu nchini kwa kutayarisha video ya Jikubali ya Ben Pol na Amani ya Moyo ya Feza Kessy, Nisher.

“Congrats to my Big Boss “Ray The Greatest” kuwa na Camera Rig Kali!! Camera ni Canon But Hiyo Rig (Nyumba) yake ni ya ukweli sana na inasaidia kurahisisha kazi iwe nzuri na ya Ki-professional zaidi. Kwenye Google inapatikana sehemu nyingi ila kwa haraka kuna jamaa wanaitwa “Redrock Micro”…check website yao…kama wewe ni director wa Video/Films/Commercials na unapenda kazi yako agiza vitu vikali,” ameandika Nisher.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents