Habari

Ray C agombana Kenya

 

Msanii wa Bongo Zouk, Rehema Chalamila aka Ray C, amejikuta katika ugomvi mkubwa kati yake na promota na mwanasiasa maarufu wa Kenya almaarufu kama Sadat.

Sadat alimpangia Ray C kufanya tour ya Kenya kwa kuanzia Nakuru, ambapo ugomvi wao ulizuka wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa habari zilizotufikia hapa Bongo 5, Ray C alidai kuwa promota huyo alikuwa akimatamani kimpenzi na kufikia kitendo cha kumtumia ujumbe kwa simu zilizomfanya muimbaji huyo kushangazwa na tabia ya promota huyo.‘Sadat alizidi kuonyesha hasira na kukerwa pale ambapo nilienda Nairobi na Boyfriend wangu Lord Eyes. Alionyesha wazi kutokufurahishwa kwa Lordi kuja na mimi kwenye show Nairobi. Hakunilipa hela ya advance nilipofika kama tulivyokuwa tumekubaliana na hata mpaka sasa, bado namdai’.

Kwa upande mwingine, Sadat amesema kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumtongoza mwanamuziki huyo na kama angekuwa na tatizo na Lord Eyes kama anavyodai Ray C, basi asingemlipia ticket ya ndege waje wote kwenye Tour hiyo.Aliongezea kuwa Ray C alikuwa kama mlevi  kabla ya show yake na iifikia hatua alilazimika kumfuata stegini na kumuondoa msanii huyo kwani angejiabisha.

Sadat amefuta maonyesho yote ya Ray c Kenya na mpaka dakika za mwisho, Mwanamuziki  huyo na meneja wake wa Kenya Maleek Buddy wamepeleka  malalamiko polisi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents