Burudani

Ray C ammshauri ex wake Lord Eyez abadilike ‘karibu kwenye tiba ya Methadone’

Baada ya Lord Eyez kutuhumiwa kwa wizi wa Laptop jijini Arusha, aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Rehema Chalamila aka Ray C amemtaka Lord Eyez kubadilika na kujiunga na tiba za kuondokana na uraibu wa madawa ya kulevya.

page

“Badilika babaa,” Ray C amesema kwenye Instagram. “Nakuombea sana ujitambue na ubadili mwendo wa Maisha yako…Wewe bado ni kijana mdogo sana na una kipaji cha pekee…..Kila Mtu Ana changamoto yake ya maisha,angalia wapi ulipokosea,litambue tatizo halafu kubali kwamba una tatizo then rekebisha Hilo tatizo,Anza Maisha mapya,Badilika………Majanga yote yanayokukuta ni ishara tosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba unakoelekea siko,Kama una akili timamu basi utagundua Hilo na utajirekebisha babaa,Nakuombea kila la kheri katika mabadiliko ya Maisha yako………..Karibu Kwenye Tiba ya Methadone……………….Methadone Kiboko ya Madawa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents