Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu kumshukuru kwa msaada

Nyota wa bongo fleva Rehema Chalamila, ambaye inasadikika kukumbwa na madawa ya kulevya, leo amemtembelea Rais wa jamhuri wa Muungano, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kumshukuru kwa msaada aliopata kutoka kwake alipokuwa na hali mbaya kutokana na matumizi hayo.

Ray C alisindikizwa na Mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve pamoja na dada yake Sarah Mtwere.

Ukitazama katika picha, Ray C anaonekana kuwa na afya nzuri. Tuendelee kumuombea arudi katika hali yake ya zamani na aishi maisha marefu.

Ray C amekuwa na mchango mkubwa sana katika tasnia ya muziki nchini na bado anahitajika, na ni kati ya majina yanayokitokeza haraka haraka ukiongelea kina dada walioikuza bongo flava.

Thank you Mr. President and Ray C we love you!

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW