Burudani

Ray C anakuja na taarab, asema Khadija Kopa ajiandae

Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na nyimbo za taarab, huku akimtaka Khadija Kopa ajiandae.
Ray C

Akizungumza na Sporah Show hivi karibuni, Ray C amesema kwenye albam yake ambayo inakuja hivi karibuni kunamchanyiko wa nyimbo mbalimbali zikiwemo taarab na zakihindi.

“Nimefanya taarab kama mbili na zook, yani nimebadilishika kabisa, kuna kwaito , kuna bongoflave ,uwindi hindi kidogo, taarab nimeimba pia ,kwaiyo Khadija Kopa ajiandae”Alisema Ray C.

Pia Ray amedai kuwa aina ya muziki anaokujanao kwa sasa hivi ni ule wa kuonyesha kipaji chake zaidi cha kuimba na siyo kucheza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents