Burudani

Ray C ang’aka kuhusu Bangi

Msanii mahiri wa muziki wa Bongo flava nchini, Rehema Chalamila, a.k.a Ray C hivi karibuni aligeuka mbogo baada ya kuulizwa na Paparazi kuhusu tuhuma za yeye na mpenzi wake wa zamani, Waziri Isaac Makuto, ‘Lord Eyez’ kutumia bangi na kana kwamba ndiyo chanzo cha kuachana kwao.

Ray C alifikia hatua hiyo alipokuwa akiongea na mmoja wa mapaparazi jijini Dar-Es-Salaam ambapo alipotakiwa kutoa ‘stetimenti’ juu ya kile kinachodaiwa kuwa, isingekuwa mpenzi wake kutumia ‘sigara kubwa’ hadi leo wangekuwa wanaitana ‘sweet bebi’.

Katika hali ya kushangaza, mwanadada huyo ambaye pia hujulikana kama ‘Kiuno bila mfupa’ alimjia juu Paparazi huyo huku akionekana kukerwa na aina ya swali aliloulizwa ambapo bila simile alianza kumwaga mvua ya maneno machafu.

“Mimi sipendi ushe***, suala la mimi kuachana na mchumba wangu ni siri yetu… kwanini mnafuatilia sana maisha yangu nyie wa*****,” alibwatuka Ray C.
Hata hivyo kwa kutumia busara, mwandishi aliamua kuwa mpole kwani alishindwa kuelewa sababu ya msanii huyo kugeuka mbogo wakati swali aliloulizwa lilistahili jibu fupi tu na la kueleweka.

Miezi michache iliyopita, mwanamuziki huyo aliachana na mpenzi wake wa muda mrefu Lord Eyez, huku habari zilizonyuma ya pazia zinasema kwamba chanzo cha wawili hao kupigana kibuti ni madai ya mwanaume kutumia ‘mjani’ kupita kiasi.

Juhudi za mwandishi wetu kumpata Lord Eyez ili kusikia kauli yake juu ya madai hayo, ziligonga mwamba kwani alipotafutwa kwa njia ya ‘kilongalonga’ chake cha mkononi hakuweza kupatikana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents