BurudaniHabari

Ray C awafata walio kwa Bush!

Ray CMwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye hivi sasa yuko kwa mzee Bush (USA) kwa ziara ya binafsi ya kibiashara pamoja na kimuziki anatarajia kufanya maonyesho kazaa

Ray CMwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye hivi sasa yuko kwa mzee Bush (USA) kwa ziara ya binafsi ya kibiashara pamoja na kimuziki anatarajia kufanya maonyesho kazaa nchini humo ndani ya mwezi ujao.

 

Akidodosa moja kwa moja kutoka huko,mwanadada huyo alisema kama mungu ataweka mambo kama yalivyopangwa…basi tarehe 3 Feb anatarajia kufanya onyesho zito ndani ya jiji la New Jersey na kumalizia na show kali litakayofanyika Washington DC siku ya tarehe 9 ya mwezi huohuo.

 

Kwa mujibu wa mwanadada huyo ambaye kuna wakati alibatizwa jina la ‘Kiuno bila mfupa’ kutokana na minenguo yake,show ya New Jersey imefanikishwa na mwanadada mtanzania aliyemtaja kwa jina la Mariam,wakati ziara ya washington Dc imefanikishwa na kampuni ya Umoja Entertainment.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents