Burudani

Ray C naye anaamka tena, kila ahusikaye ashiriki kumshika mkono

Kuna msemo unaosema ‘uimara na uthabiti wa mtu haupo katika kuweza kuishi katika misingi aliyojiwekea ila uimara na uthabiti ni vile anavyoweza kurudi katika ile misingi alojiwekea baada ya kuteleza.’

Kiuno bila mfupa na mvuto wa kipekee ambao umeimbwa na kutajwa na wasanii mbalimbali kila walipokuwa wakizungumzia mwanamke mzuri ilikuwa ni macho na kiuno kama Ray C, mwanadada aliyekuwa na uwezo wa kunyonganyonga mauno yake kana kwamba mfupa sio moja ya kiungo katika mwili wake.

Sauti tamu iliyokuwa ikisika maridhawa kwenye midundo yenye ladha ya Asia. Ni mwanamke gani kipindi hicho angeambiwa ana kiuno kama cha Ray C asibaki ana tabasamu usiku kucha?

Inatokea kwa wanadamu tunafanya makosa,tunateleza iwe kwa kujua au kwa kutokujua. Ilitokea kwa mwanadada Ray C, kwa sababu mbalimbali alijikuta akiangukia sehemu ambayo haikuwa salama kwake, afya na career yake kwa ujumla.

Yaliyotokea yakatokea Na the rest is history na haina maana tena ya kuikumbuka kwa kuwa haimsaidii kumfanya awe yeye tena. Zaidi ni kukumbuka kuwa ilikuwa ni mbaya na hatakiwi kurudi tena.

Good news ni kuwa Ray C is back. Tena mara hii akirudi kama Ray C yule tulomzoea kwa muonekano na mvuto uleule. Ni wazi kila mmoja amemmis. Nani hakumbuki ‘Nataka Niwe Nawe Milele’, ‘Uko Wapi’, ‘Umenikataa Bila Sababu’,Sogeasogea na ngoma nyingine kali za mwanadada huyu?

Dada yangu Ray C, tasnia,wasanii wenzako na mashabiki wamekumis wanatamani kukuona tena. Kwa vipande vidogo tunavyosikia sauti yako bado ina mvuto uleule na sina mashaka na nyonga yako isiyo na mfupa. Ni wewe tu kuona una deni na kila sababu ya kuburudisha watanzania. Tamani kushinda Ninaamini macho na masikio ya watanzania yapo tayari kuona ukikonga nyoyo zao kwa mara nyingine.

Kwa wadau wa muziki na wengine wanaohusika, Ray C anahitaji msaada wenu wa hali na mali. Kusaidia yeye kurudi sio tu mtakuWa mmerudisha burudani maridhawa kwa Watanzania bali mtakuwa mmesaidia mamia ya mabinti wadogo kuamini haijalishi taswira imechafuka kiasi gani unaweza ukarudi na thamani yako ikawa juu zaidi.

By Eliezer Gibson ‘Greencitynative
Intargram:@gibson_elly
Email:[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents