Bongo Movie

Ray Kigosi aitaka Serikali kupiga stop TV zinazoonesha filamu za nje

Msanii wa Bongo Movie, Vicent Kigosi ‘Ray’ ameishauri Serikali kuvizuia vituo vinavyorusha Filamu na Tamthilia za kigeni kwa kuzitafsiri kwa lugha ya kiswahili kwani kufanya hivyo ni kusambaza content zenye maadili ya kigeni.

Ray Kigosi

Ray amesema kitendo cha kutafsiri tamthilia hizo ni kusambaza tamaduni za kigeni lakini pia kunaathiri filamu za ndani kwani kuna kuwa na ushindani mkubwa hata wale wasio kuwa na uelewa wa lugha za kigeni hupata urahisi wa kufuatilia tamthilia hizo kitu ambacho kinaua soko la filamu za nyumbani.

Hii sio haki kabisa serikali yetu ichukue hatua mapema!!…TVs za nchini India hazirushi films wala series za kimarekani au kizungu kwa lugha ya kihindi na kinyume chake. Dubbed films za Hollywood zinaonyeshwa tu kwenye majumba ya cinema nchini India na sio kwenye DVD au TVs na kinyume chake. Lengo Ni kulinda soko la ndani na wasanii wa ndani na hii ndio Sababu licha ya Hollywood Kuwa na kazi bora na teknolojia ya juu zaidi but India nayo imeweza Kuwa mpinzani wake mkubwa kwa sera nzuri za kibiashara kwa wote“,ameandika Ray Kigosi kwenye ukurasa wake wa instagram huku akiendelea kuhoji.

Sasa nashangaa kwanini serikali ya Tanzania imeruhusu films na series za nje kurushwa kwa Kiswahili tena kwa kuanzishwa tv maalum za contents za kazi za nje kwa Kiswahili ? This is not fair kabisa kwa industry na wasanii wa Tanzania tena sisi tukiwa bado tuko nyuma kuliko wao mpaka Kiuchumi kwa ujumla Kama taifa 
Mbaya zaidi hizi series za kikorea, kichina, kihindi na hata kizungu zinazoruka nchini wanaorusha wanaonekana hawana mikataba na producers wa nchi husika na hata ajira hawatoi za kueleweka kwa watanzania tofauti na kazi zinazotengenezwa na watanzania wenyewe hutoa ajira nyingi“,ameandika Ray Kigosi.

Akitolea mfano Kampuni ya Sony ambayo ina zaidi ya channel 3 nchini India, Ray amesema Kampuni hiyo inaonesha filamu na Tamthilia za Hollywood nchini India bila kutafsiri kwa kihindi hii yote ili kulinda soko la ndani la filamu za Bollywood.

Sony Pictures ya Hollywood kwa mfano Inamiliki vituo vya TVs zaidi ya 3 nchini India but vyote hurusha original contents I mean series na movies za Bollywood na sio kazi za Hollywood kwa lugha ya kihindi. Lengo Ni kulinda soko na ajira za wasanii Wazawa“,ameandika Ray Kigosi.

Hata hivyo, Ray Kigosi ameishauri Serikali kwa kuhoji kwanini iviruhusu vituo vya TV vilivyopo nchini kuonesha vilamu za kigeni kwa kutafsiri kwa kiswahili huku akiita kitendo hicho ni kama kosa la kuhujumu uchumi na kuiomba Serikali ipige stop matangazo hayo ili kulinda soko la filamu za ndani .

Sasa kwanini wizara na serikali yetu imekubali kuwaumiza na kuwaonea wasanii wa Tanzania na hata kudidimiza uchumi wa Tanzania !! Maana Hadi sasa wasanii wa Tanzania ndio wanakamuliwa makodi mengi kuliko hizi kazi za nje zinazoonyeshwa kiujanjaunja na na kinyume na Sheria za nchi husika, hiyo Tisa, kumi sasa hivi kazi za Wazawa zikiwemo series hata kuchukuliwa kwenye vituo vya TVs nchini Ni shida, sababu wanaonyesha kazi za kikorea, kichina, kihindi bure na watanzania hata wasiosoma vizuri wanaelewa sababu zimetafsiriwa kwa Kiswahili, Rai yangu wadau wasimame kidete sera ya filam ipatikane hizi Tvs za aina hii zipigwe stop badala sera iwatake watengeneze contents za kiswahili kwa kutumia Wasanii wa Tanzania warushe katika hizo Tvs zao sio ujanja wa kuhujumu uchumi na kueneza utamuduni wao.“ameandika Ray Kigosi.

Ray Kigosi ni moja ya Wasanii wa Bongo Movie ambao waliandamana mwezi wa Aprili mwaka huu kupinga uingizwaji kiholela wa filamu za kigeni.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents