Burudani

Rayvanny wa WCB Kuwania tuzo za kimataifa za BET

By  | 

BET ni moja kati ya tuzo ambazo zinazofuatiliwa kwa ukaribu na watu wengi duniani. Kwa mwaka huu msanii kutoka WCB, Raymond amefanikiwa kupata bahati ya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava aliyechaguliwa kuwakilishi katika tuzo za BET.

Msanii huyo anawakilisha Tanzania kwenye kipengele cha International Viewer’s Choice Awards ambacho msanii aliyepigiwa kura nyingi na mashabiki ndio hushinda. Wasanii wengine wanaowania tuzo hiyo ni Dave (Uingereza), Amanda Black (SA), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica), mwaka jana ilinyakuliwa na Falz wa Nigeria.

Wakati huo huo katika kipengele cha Best International Act: Africa ambayo ndio tuzo inayowaniwa na wasanii wa Afrika inatarajiwa kushindaniwa na Wizkid, Davido, Tekno, Mr Eazi (wote kutoka Nigeria), Stonebwoy (Ghana), na Nasty C, Babes Wodumo na AKA (wote kutoka Afrika Kusini).

Beyonce ndio anaongoza kwa kuwania tuzo nyingi kwa maka huu ambazo ni saba akifuatiwa na Bruno Mars anayewania katika vipengele vitano.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Juni 25 ya mwaka huu katika ukumbi wa Microsoft Theater mjini Los Angeles.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments