Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Rc Ayoubu wa Mjini Magharibi ataja sababu za kufanikisha waliyoshindwa viongozi waliopita

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahamudu ametaja sababu za yeye kuweza kufanikisha mambo ambayo viongozi waliopita katika mkoa huo walishindwa kuyafanya ikiwemo ujenzi wa madarasa ya wanafunzi ambayo yaliyotelekezwa kwa zaidi ya miaka mitano.

Akiongea na Bongo5 kiongozi huyo amesema, moja ya jambo lililosababisha kwa viongozi wengine kushindwa kumilisha baadhi ya maendeleo ya jamii ni kutokana na mazingira hayakuwa rafiki kwa uongozi hao katika eneo hilo ila yeye ataweza kujenga kutokana na kuwa amejiandaa kikamilifu.

“Waliotoka pengine hawakushindwa kujenga ila kutokana na kuwa mazingira haya kuwa rafiki ndio maana wameshindwa kumalizia ujenzi huo ila kutokana na kuwa mazingira niliyopo ni rafiki hivyo sitoshindwa kukamilisha,” amesema Rc huyo.

Vile vile amewasisitiza watu wa Zanzibar kuhakikisha wanashiriki katika ujenzi kwa kutoa vitu na si fedha.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW