Habari

RC Chalamila awafukuza wanafunzi 7 kwa tuhuma za kuchoma mabweni ‘Hawatafanya mtihani kwa miaka mitano’

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila ametangaza kuwafukuza Shule wanafunzi 7 wa kidato cha sita, katika Shule ya Sekondari Kwanja iliyopo Chunya mkoani Mbeya, Waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kuchoma moto mabweni.

RC Chalamila ametoa maamuzi hayo leo Oktoba 23, 2019, akiwa Shuleni hapo wakati akitoa ripoti kuhusiana na tukio la kuwasimamisha shule wanafunzi waliohusika kuchoma mabweni shuleni hapo ambapo wote waliohusika kwenye vurugu hizo walitakiwa walipe faini ya Shilingi 200,000/= kwa kila mmoja, na faini ya Shilingi laki 5 kwa kila aliyechoma moto mabweni hayo.

Wanafunzi hao 7 waliofukuzwa watafunguliwa mashtaka mahakamani na hawataruhusiwa kufanya mtihani wa Taifa kwa miaka mitano.

Nimewatimua wanafunzi wote ambao hawajalipa faini na nitaandika ripoti kwenye mamlaka husika kuwazuia wasifanye mitihani tena kwa muda wa miaka 5, na kama kuna shule yeyote itawapokea itakuwa hatarini. Nawambieni jinsi ya kuwafuatilia hawa wanafunzi ni ndogo sana, Kwa sababu tunawafahamu tangu walipoanzia mpaka wapo sasa na uzuri zaidi tumewalipia ada wenyewe wala hawatusumbui kuwapata,” Amesema RC Chalamila.

Mapema mwezi huu wa Oktoba Mkuu huyo wa Mkoa, Aliwaadhibu wanafunzi hao kwa kuwacharaza bakora na kisha kuwasimamisha masomo wanafunzi wote waliohusika kwenye vurugu na kuchoma mabweni hayo na kuwataka wakirudi shuleni hapo warudi na faini kwa ajili ya ukarabati wa mabweni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents