Habari

RC Chalamila awataka wafanyabiashara na waajiri kuzingatia usalama na afya kwa wafanyakazi (+Video)

Mkuu wa mkoa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewataka wafanyabiashara na waajiri nchini kuhakikisha wanazingatia suala la usalama na afya kwa wafanyakazi kwani ni sekta muhimu katika
kuweza kufikia uchumi wa kati hivyo wanapaswa kuyaelewa.

Mhe. Chalamila ameyasema hayo jijini Mbeya wakati akifungua Semina maalum kwa waajiri wa
mkoa wa Mbeya kuhusu kampeni maalamu ilioanzisha na OSHA kwa lengo la kupnguza Ajali na
magonjwa sehemu za kazi.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa usalama na Afya, Alex
Ngata amesema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kuendelea kutoa elimu ya usalama na
afya kwa wafanyabiashara hao kupitia kampeni ya vision zero.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mfunzo, utafiti na takwimu Bwana Joshua matiko amesema, sekta
ya uzalishaji ndio inayoongoza kwa kusababisha ajali, ikufuatiwa na sekta ya ujenzi, na ndio maana
wakaamua kuja na program maalamu ya kuelimisha juu ya kupunguza ajali na magonjwa sehemu za
kazi

Na kwa upande wao washiriki wa semina hiyo wamesema mafunzo hayo yatasaidia kuweka mifumo
ambayo itawasaidia kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali sehemu kazi kwani jambo
hilo litawezekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents