Habari

RC Gambo akabidhi milioni 23 kwa manusura wa Lucky Vicent

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabidhi jumla ya shilingi milioni 23 kwa familia tatu za manusura wa ajali ya watoto wa Lucky Vicent ambapo kila mzazi amepata milioni 7.75 bila kupewa masharti yoyote.

Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari ambapo kila mzazi amepata Milioni 7.75, Gambo amesema fedha hizo zilikuwa Zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva.

“Kwa niaba ya mkoa wa Arusha tuwapatie nyinyi kama wazazi nyie nyie mtaangalia ni busara gani kama mtatumia kuwauguza watoto wetu hiyo ni kazi yenu, kama mmeamua kuitumia kuingiza kwenye mfuko wa elimu kwaajili ya watoto wetu hiyo ni kazi yenu tulibakiwa na kiasi cha fedha cha Milioni 23 laki mbili na 73 na mia nane na 85 na tumeamua kuigawanya kwa tatu kiasi hicho ambacho leo kila familia itapata milioni 7 laki 7 na elfu 50,” alisema Gambo.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa

Katika hatua nyingine, Gambo alisema Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto hao ili kuwaweka sawa na kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la 7 unaowakabili mnamo mwezi Septemba.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents