Habari

RC Gambo hakuogopa kuwa muongo madhabahuni aliniita mimi rafiki yake – Mh. Lema

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema baada ya kutambulishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo kuwa ni rafiki yake katika Ibada ya kusimikwa Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha.

.

Mbunge huyo wa Arusha hajasita ameweka wazi jinsi alivyotambulishwa na Mkuu wa mkoa huo, Lema ameeleza kuwa RC Gambo hakuogopa muongo madhabahuni kwa kumtambulisha kuwa yeye ni rafiki yake.

“Ktk Ibada ya kusimikwa Askofu,Mh Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki.Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena.Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana.Mrisho Gambo(RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake,” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents