Burudani ya Michezo Live

RC Kilimanjaro aagiza DED wilaya ya Mwanga asilipwe mshahara kwa kushindwa kujibu swali hii

RC Kilimanjaro aagiza DED wilaya ya Mwanga asilipwe mshahara kwa kushindwa kujibu swali hii

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameziagiza mamlaka zinazohusika kumlipa mshahara Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga Zefrin Lubuva, kutomlipa mshahara wake wa Februari baada ya kushindwa kujibu swali alilomuuliza.

RC Mghwira ametoa agizo hilo leo Februari 14, 2020 katika kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa cha makisio ya Mpango wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021, na ndipo alipohoji sababu iliyopelekea Manispaa hiyo kushindwa kutimiza lengo la kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Mkurugenzi wa Mwanga kila wakati umekuwa ukishindwa kujibu maswali vile inavyopaswa, sijajua ni nani anakulipa mshahara, ila mamlaka inayohusika kukulipa isikulipe mshahara wa mwezi huu” amesema RC Mghwira.

Chanzo Eatv.tv.
By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW