HabariUncategorized

RC Makonda aendelea kuzibana mbavu kampuni mbili za ukandarasi Dar

Kongamano la tathimini ya hali ya miondombinu ya jiji la Dar es salaam lililoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda limefanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre Posta ambapo tayari baadhi ya wakandarasi wa wilaya ya Ilala, Temeka pamoja na Kinondoni wametoa maelezo yao juu ya ubovu ya barabara zao.


RC Makonda akiwa kwenye mazungumzo na wadau wa barabara Dar es salaam.

Aidha mkuu huyo ameendeleza msimamo wake wa kuzifukuza ndani ya mkoa wa Dar es salaam kampuni mbili za ukandarasi ambazo ni Skol Building Contractors Ltd pamoja na Del Monte Construction kwa madai zimejenga barabara nyingi chini ya kiwango.

Madiwani pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa ambao walipata fursa za kuzungumza kuhusu changamoto za barabara, walisema changamoto za ubovu wa barabara ndani ya mkoa wa Dar es salaam unasabishwa na ufinyu wa bajeti pamoja na usufumbufu wa baadhi ya wakandarasi ambao wamekuwa akipewa tenda katika maeneo hayo.

Akiongea na wananchi pamoja na wakandarasi waliojitokeza katika kongamano hilo, RC Makonda amesema barabara nyingi za jiji la Dar es salaam ni mbovu huku akidai wakandarasi pamoja na wataalam ya tathimini ndio watu ambao wanasababisha tatizo hilo.

“Lengo la kongomano hili ni kutaka tuwafahamu wataalamu wetu wa barabara, wataalum wetu watambuane na Dawasco pamoja na wadau mbalimbali kwa sababu kuna wakati hizi taasisi zinaingiliana, huwezi kukarabati barabara bila kujua miundombinu ya maji,” alisema RC Makonda.

Aliongeza, “Kama unapokea hela ambayo haifanyi kazi wewe ni mwizi, wakandarasi wanashindwa kusimamia barabara, watu ambao wanasababisha ubovu wa barabara ni hawa wakandarasi sio CCM wala watu wengine. Kila mwaka mnatengeneza barabara, kila mwaka mna bajeti ya kukarabati ya barabara halafu barabara hizo bado zinaendelea kuwa mbovu kila siku,”

Kufuatia changamoto ya mabomba ya maji yaliyopasuka na kusababisha kero ya kumwagika kwa maji katika makazi ya watu, mkuu huyo amewataka Dawasco kutatua changamoto hizo pamoja na kuunda utararibu wa kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ambayo mabomba yamepasuka.


DC wa Ilala, Sophia Mjema

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents