Burudani

RC Makonda aibuka upya, aahidi kumfunga Lemutuz, Majizzo na Meya Kinondoni endapo hawatafunga ndoa mwaka huu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda amethibitisha ndoa ya Mkurugenzi Mtendaji na Muanzilishi wa kituo cha Radio EFM na TVE, Francis Ciza maarufu kama DJ Majizzo  na Muigizaji wa filamu, Lulu ambapo amesema mipango ya harusi ya wawili hao tayari inafanyika na huenda mwaka huu ndoa hiyo ikafanyika.

Image result for rc makonda
RC Paul Makonda

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye tamasha la Komaa Concert jana jijini Dar es salaam, RC Makonda amesema kuwa kutokana na imani yake hataki kuwaona marafiki zake wanakuwa mabachela na kuahidi kuwafunga jela endapo watakiuka ahadi zao za kuoa.

Akitaja marafiki zake amesema watu hao ni Majizzo, Lemutuz na Meya wa Kinondoni ambapo amewataka mwaka huu waweke mipango yao sawa ya harusi ili wafunge ndoa.

Nina ndoa kubwa tatu lazima nizisimamie na wasipooana nawafunga, moja ni Majizzo unajua mimi ni mkristo kwenye Biblia inasema wengine wataokolewa kwa moto. Sasa Majizzo tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu wameshakuja nyumbani tumeshafanya vikao vingi vya kupanga harusi. Lakini kuna harusi nyingine ya Meya wa Kinondoni nimemwambia na yeye asipooa namfunga. Lakini kuna Lemutuz naye asipooa namfunga. Kwa hiyo kuna watu watatu hawa lazima mipango yao ya harusi ikamilike mwaka huu na waoe,“amesema RC Makonda.

Ndoa kati ya Lulu na Majizzo imekuwa ni tetesi ya muda mrefu ambapo wawili hao hawajawahi kujitokeza popote kuzungumzia suala hilo.

Related Articles

9 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents