Habari

RC Makonda akagua ujenzi wa daraja jipya la Selander ambalo ni kubwa kuliko daraja la Nyerere (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 19 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja jipya la Selander linalopita katikati ya bahari lenye urefu wa Km 1.03 likiunganisha eneo la Agha Khan na Coco Beach ambapo ujenzi wake umegharimu dola za kimarekani milioni 112 sawa na Bilioni 256.

RC Makonda ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao kukamilika kwake itakuwa neema kubwa kwa wananchi kwakuwa litasaidia kupunguza tatizo la msongamano wa Magari ambalo licha ya kurudisha nyuma maendeleo pia limekuwa kero kwa wananchi.

Miongoni mwa mambo yaliyomfurahisha RC Makonda ni kuona vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi huo vinatoka kwenye viwanda vya ndani, ajira kwa vijana wazawa na pia uwepo kampuni za kitanzania zilizopata tenda ya ujenzi kwenye mradi huo jambo linalosaidia kuinua uchumi wa Taifa.

Hata hivyo RC Makonda amesema Daraja hilo lina urefu wa mita1,000 na upana wa mita 20.5 na litakuwa na njia 4 za magari na njia 2 za watembea kwa miguu pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa Km 5.2.

Kwa upande wake mtendaji Mkuu wa TANROAD Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja la muda utakamilika ndani ya mwezi huu na ujenzi wa daraja kubwa utakamikika kabla ya October 14 mwaka 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents