Habari

RC Makonda amgeuzia kibao Diamond na wanaume wengine matapeli wa kuoa, Ataka wanawake waliodanganywa kuolewa wakamshtaki (+video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka wanawake wote ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam ambao wamedanganywa kuolewa na kisha kukimbiwa na wanaume, Waende mahakamani kudai haki zao ili kukomesha tabia ya udanganyifu kwenye mahusiano.

RC Makonda amesema hayo leo Agosti 20, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari, Ambapo amesema kuwa anakuja na mpango wa kujadili kwa kina tatizo la wanaume kuwadanganya wanawake kwa ahadi za kuoa na kisha kuwakimbia.

Makonda amesema anaamini wanawake wengi kwasasa wameumizwa kisaikolojia, Jambo linalopelekea wanawake kuwachukia wanaume na wengine kukataa hata kuolewa kabisa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents