Tupo Nawe

RC Makonda amuomba Rais Magufuli kuwapatia JWTZ mradi wa NSSF unaosusua kwa miaka 15 (Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kuwapati JWTZ mradi wa ujenzi wa Nyumba za NSSF zilizopo kata ya Toangoma ambazo ujenzi wake umesuasua zaidi ya Miaka 15 jambo linaloisababishi serikali hasara.

RC Makonda amesema anaamini kwa utendaji kazi wa vijana wa JWTZ utawezesha majengo hayo kukamilika ndani ya muda mfupi na kuanza kutumiwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kuendelea ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambao Leo ilikuwa zamu ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Majengo 12 ya Magereza Ukonga ambayo hivi karibuni Rais Magufuli aliwany’anyanya TBA baada ya kusuasua na kuamua kuwakabidhi JWTZ na sasa ujenzi unaenda vizuri.

Hata hivyo RC Makonda amewapongeza JWTZ kwa kasi kubwa wanayoonyesha katika mradi huo na kueleza kuwa anaamini watakamilisha ujenzi ndani ya muda uliokusudiwa.

Kwa upande msimamizi wa ujenzi huo Bigedia Charles Mbuge amesema ujenzi wa majengo hayo utakamilika na kukabidhiwa ndani ya miezi miwili na nusu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW