Tupo Nawe

RC Makonda amuwashia moto Meya wa Ubongo (Video)

Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob leo ameumbuliwa hadharani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya meya huyo kukosa nidhamu kwa kudanganya wananchi kuwa yeye ndio amefanikisha mradi wa ujenzi wa Kisima ca Maji Kata ya Mbezi Makabe wakati Rais Dkt.John Magufuli ndio alietoa fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 611 kwaajili ya kumaliza kero za maji kwa wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa mwendelezo wa ziara ya ukaguzi miradi ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam ambapo RC Makonda ameshangazwa kuona Meya anajinadi mbele ya wananchi na viongozi kuwa yeye ndie aliefanikisha upatikanaji wa fedha hizo na ndio alieweka saini badala ya kumshukuru Rais Dkt. John Magufuli alietoa fedha hizo.

RC Makonda amesema kitendo hicho ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wanaotoa fedha kwaajili ya kutatua kero za wananchi ambapo amemtaka Meya huyo kuwa na shukrani kwa viongozi bila kujali itikadi za kisiasa.

Mradi wa ujenzi wa kisima cha Maji Mbezi Makabe unagharimu zaidi ya Shilingi Million 611 zilizotolewa na Rais Magufuli na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya Wakazi 75,000.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW