Habari

RC Makonda amvaa mwanafunzi aliyedaiwa kutekwa ‘wakimalizana nae Iringa watuletee Dar’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewashangaa baadhi ya watu wanaochafua mkoa wa Dar es salaam kwa kusema kuwa hakuna ulinzi na usalama ile hali mkoa kwa sasa upo salama ukilinganisha na miaka ya nyuma.

RC Paul Makonda

Akizungumza leo Machi 09, 2018 kwenye sherehe za kuwatunuku vyeti askari waliofanya vizuri mwaka jana katika chuo cha maofisa polisi jijini Dar es salaam, ametaja baadhi ya matukio ambayo yanauharibu mkoa likiwemo la Mwanafunzi wa Chuo cha UDSM, Abdul Nondo ambaye alipotea Jumanne ya wiki hili jijini Dar es salaam, na kupatikana huko mkoani Iringa.

RC Makonda amesema matukio kama hayo yanaharibu sifa ya mkoa kwani hayana uthibisho kama alitekwa au alilala kwenye gari akajisahau ikizingatiwa kuwa ni kipindi cha vyuo kufungwa.

Soma zaidi – Jeshi la Polisi Iringa lamshikilia Abdul Nondo kwa uchunguzi kujua kama kweli alitekwa

Kufuatia tukio hilo, RC Makonda amemtaka Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amchukue mwanafunzi huyo kwa mahojiano zaidi akishaachiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa ili kujua undani wa tukio hilo huku akiwaonya waandishi wa habari kuzingatia miiko ya urushaji wa habari kama hizo zinazoleta taharuki kwenye jamii.

Juzi nilisikia sikia kuna mmoja amesema ametekwa, mimi nafikiri wakimalizana nae kule Iringa watuletee hapa Dar es salaam wasituchafulie mkoa wetu, na wengine wanaokimbia kuandika andika bila hata kuwa na ushahidi ya kwamba mtu ametekwa. wewe watu wamefunga chuo wanarudi majumbani kwao hali imepoteza Network tu huko njiani fulani hatumuoni ametekwa ita waandishi wa habari toa kauli.!! Ifike hatua niwaombe Waandishi wa Habari angalieni taarifa mnazozipeleka kwa umma, kama hazijathibitishwa na mamlaka husika achaneni nazo,“amesema RC Makonda.

Soma na Hii – Jeshi la Polisi limesema matukio ya mauaji yamepungua nchini

Kwa upande mwingine RC Makonda amemtaka Kamanda Mambosasa kushungulikia watu wote wanaotoa lugha za matusi kwa viongozi wa serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents