Habari

RC Makonda anatakiwa afukuzwe Kazi, hatutashiriki tena uchaguzi – Mhe. Mbowe (+video)

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda hatakiwi kukemewa bali anapaswa afukuzwe kwazi mara moja kwani anakiuka maadili ya kazi yake.

Freeman Mbowe

Mbowe akiongea na Waandishi wa Habari Leo Septemba 19, 2018 jijini Dar es salaam amedai kuwa kitendo cha RC Makonda kuwapongeza Askari Polisi baada ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga sio kitendo cha kuvumiliwa wala kukemewa bali ilitakiwa aachishwe kazi.

Kwa upande Mwingine Mbowe amesema kuwa CHADEMA imejitoa kwenye chaguzi zote ndogo zinazotangazwa nchini na badala yake watakuwa wanajifua kwa kujenga chama hicho hadi mwaka 2020.

“Kamati ndogo ya Kamati Kuu imekaa na kufikia maamuzi ya kutoshiriki chaguzi zilizotangazwa na kwasasa na badala yake tutapeleka nguvu kubwa kwenye oparesheni za kukijenga Chama kuliko kupoteza rasilimali nyingi, hatutashiriki chaguzi sio tu za Ubunge hadi za Madiwani,” Freeman Mbowe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents