Habari

RC Makonda apokea neema kutoka kwa waalimu 18 kutoka Marekani

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam, Paul Makonda Alhamisi hii amekutana na wadau elimu 18 kutoka nchini marekani ambao wapo hapa nchi kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo utamaduni, lugha ya Kiswahili itakayo wasaidia katika kuandaa mitalaa yao.

RC Makonda akizungumza mbele ya waandishi wa habari.

Walimu hao ambao wakiongozwa na Dr Fredoline kutoka American Institute of Human Resource Development pamoja coordinator wa msafara huyo, Shannan Akosua Magee kutoka shule ya Albany Community Charter Schools, wapo katika hatua za mwisho za kumaliza mafunzo yao.

Miongoni mwa masuala waliyozungia wakati wa mkutano wao huo ni pamoja na kuangalia namna ya kujenga maktaba ya jamii mkoani Dsm ambayo itawezesha wananchi kupata fursa ya kujisomea na kuelewa utamaduni wa nchi hiyo na ndani ya nchi.

Kufuatia mikakati hiyo ya ujenzi wa maktaba, Makonda amewahimiza wananchi wa mkoa huo kujenga utamaduni wa kujisomea.

Jambo lingine ambalo wamelijadili ni pamoja kuangalia wanajenga vipi umoja katika kuleta walimu watakao kuja kufundisha mkoani.

Pia ameeleza kuwa walimu hao watasaidia katika kuwafundisha watanzania namna ya kufanyakazi na kufuatia utamaduni wao na kuuthamini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents