Aisee DSTV!
SwahiliFix

RC Makonda asema kuanzia wiki lijalo Wachungaji wataanza kuhubiri usiku kwenye kumbi za starehe ‘Ningekuwa Mchungaji waumini mngekula fimbo kila siku’ (+video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema kuwa atatoa kibali kwa viongozi wa dini kwenda kuhubiri neno la Mungu kwenye kumbi za starehe nyakati za usiku.

RC Paul Makonda

RC Makonda ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 8, 2019 katika Kanisa la Inuka Uangaze la Mtume  Boniface Mwamposa maarufu kama ‘Bulldozer’ lililopo Kawe, Jijini Dar es Salaam.

Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuwakumbusha watu kuwa Mungu yupo na kuacha kufuatilia mambo mengine ya kidunia ambayo hayana msaada kwenye jamii.

Kuanzia sasa nawambieni watumishi wa Mungu kama mnataka kuhubiri kwenye klabu nawapa kibali mkawahubirie huko, Angalau kwa nusu saa wapate fursa ya kusikia neno la Mungu, wasije kusema hawakusikia. Wafuateni huko… Sasa nimuone huyo mwenye klabu akatae mimi si ndio mkuu wa mkoa? Kuanzia wiki ijayo mkitaka kwenda klabu yoyote mniambie kapigeni kwa nusu saa,“amesema RC Makonda.

Kwa upande mwingine, RC Makonda amewataka wanaume kuacha vitendo vya kuwanyanyasa wanawake, Na kuwataka wajipange kwani amekuja kutatua matatizo yote yanayosababishwa na wanaume dhidi ya wanawake ikiwemo kutelekezwa.

View this post on Instagram

——————————————————————————————– Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (@baba_keagan) amesema kuwa atatoa kibali kwa viongozi wa dini kwenda kuhubiri neno la Mungu kwenye kumbi za starehe nyakati za usiku. RC Makonda ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 8, 2019 katika Kanisa la Inuka Uangaze la Mtume Boniface Mwamposa maarufu kama ‘Bulldozer’ lililopo Kawe, Jijini Dar es Salaam. Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuwakumbusha watu kuwa Mungu yupo na kuacha kufuatilia mambo mengine ya kidunia ambayo hayana msaada kwenye jamii. . . . . “Kuanzia sasa nawambieni watumishi wa Mungu kama mnataka kuhubiri kwenye klabu nawapa kibali mkawahubirie huko, Angalau kwa nusu saa wapate fursa ya kusikia neno la Mungu, wasije kusema hawakusikia. Wafuateni huko… Sasa nimuone huyo mwenye klabu akatae mimi si ndio mkuu wa mkoa? Kuanzia wiki ijayo mkitaka kwenda klabu yoyote mniambie kapigeni kwa nusu saa,“amesema RC Makonda. Kwa upande mwingine, RC Makonda amewataka wanaume kuacha vitendo vya kuwanyanyasa wanawake, Na kuwataka wajipange kwani amekuja kutatua matatizo yote yanayosababishwa na wanaume dhidi ya wanawake ikiwemo kutelekezwa. WRITTEN AND EDITED BY @mgallahtz .

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW