Habari

RC Makonda atembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole (+Picha)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Dar es salaam mapema leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya Ofisi hizo kukumbwa na janga la moto.

RC Makonda kulia akiwa kwenye Ofisi za Clouds Media Group.

Mhe. Makonda amefika Ofisini hapo kutoa pole kwa janga la moto lililoipata Ofisi hiyo siku ya jana majira ya saa nne asubuhi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar es salaam.

RC Makonda akinena jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga.

Viongozi wengine wa serikali waliofika Ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manspaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.

Hata hivyo, Tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV vimerejea hewani baada ya kupotea siku nzima ya jana kutokana na hitilafu iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents