HabariUncategorized

RC Makonda atembelewa na wawekezaji kutoka China, viwanda 200 kujengwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Alhamisi hii amekutana na ugeni wa wawekezaji kutoka China kujadilia na kuhusu mambo ya uwekezaji ambapo zaidi ya viwanda 200 vinatarajiwa kujengwa.

RC Makonda akiwa na wawekezaji hao.

Akingumza jijini Dar es Salaam leo, RC Makonda amesema miongoni mwa lengo kuu la kutembelewa na ugeni huo ni kuhakikisha mkoa wa Dar es salaam unakuwa kuwa na uwekezaji mkubwa katika kuelekea Tanzania ya viwanda.

Wawekezaji hawa wanakwenda kuwekeza Tanga na kunduchi Dar es Salaam na Wana wekeza miradi yenye thamani ya Dola bilioni 3.

Aidha amewataka wanachi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za uwekezaji.

“Sisi kazi yetu kama serikali ni kuweka mazingira ya uwekezaji na hawandugu zetu wametoka jimbo la nilizungumza nao nilipotembelea huko kwao mwakajana”Amesema Makonda.

“Naamini kwamba Rais Magufuli na RC MAKONDA watatupa kipaumbele Katika uwekezaji wetu kutokana na uhusiano mzuri uliopo naona ya nchi zetu hizi mbili”.Amesema Xiezengyi

Wachina hao wanatarajia kuwekeza Katika Mkoa wa Tanga na kuungamisha biashara zao na viwanda Kiwanda cha kunduchi ili mkoa wa Dar es salaam uweze kunufaika na uwekezaji huo wenye thamani ya dola za kimarekani Bilion Tatu.

Pamoja na hayo Makonda ameeleza kuwa Kuna clip ina zungunguka mtandaoni ikieleza kuwa Ethiopia kuwa Wana kiwanda kikubwa zaidi kuliko nchi zote barani Afrika na kusema kuwa wananchi wasihofu kwani Dar es Salaam itajenga kiwanda kikubwa zaidi ya mara tatu ya hicho chenye Siguare mita Milion Tano na uwekezaji huu utafanyika wilayani Kigamboni.

“Kuna mwekezaji mwingine ameonyesha nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari Nawaomba wafanyabiashara wetu mchangamkie fursa hizo za kibiashara na vijana pia mchangamkie fursa za ajira” Amesema Makonda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jimbo la Gwangzou , Xie zhenghy kutoka China amesema wao wako tayari kwa uwekezaji na katika nchi ambazo zitaendana kiutamaduni kama ilivyo kwa Tanzania.

Hata hivyo amesema kuwa China imekuwa na nafasi kubwa ya kuwekeza barani Afrika ambapo imekuwa na uwekezaji mkubwa nchini Misri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents