Aisee DSTV!

RC Makonda atimiza ahadi ya kumpeleka India mgonjwa Pascal wa BSS (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametimiza ahadi ya kusaidia gharama za matibabu ya mshindi wa BSS 2009 Pascal Cassian kwa kumkabidhi Tiketi ya Ndege,Pesa ya Nauli, Chakula,Hotel na Pesa ya kujikimu kwa watu wote watatu watakaomsindikiza akiwemo Mke wake na Mkuu wa kitengo cha Urolojia Hospital ya Taifa Muhimbili.

RC Makonda amesema uamuzi wa kumpeleka Nchini India ni baada ya Jopo la madaktari bingwa wa Muhimbili kuridhia na kumtafutia Hospital ya kimataifa nchini India yenye uwezo wa kutibu tatizo hilo.

Aidha RC Makonda amewashukuru watanzania wote waliochangia na kufanikisha safari hiyo na kuwaomba wazidi kuwa na moyo huohuo wa kusaidiana kwenye matatizo.

Kwa upande wake Pascal Cassian amemshukuru RC Makonda kwa kuona maumivu aliyokuwa akiyapata na kuamua kumsaidia ambapo ameeleza kuwa anaamini atarejea nchini akiwa amepona kwa uweza wa Mungu.

Itakumbukwa RC Makonda aliamua kumsaidi Pascal kwa kumtoa Nyumbani na kumpeleka hospital baada ya kuona kupitia mitandao ya kijamii maumivu aliyokuwa akiyapata baada ya kupata ajali iliyopelekea tatizo kubwa la kwenye mfumo wa figo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW