Habari

RC Makonda aunda kamati ya kuchunguza ushoga na wanaocheza movie za X ‘nimepata majina 200 ya mashoga Dar, tutawapima’ (+video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda ameunda Kamati ya watu 17 ya kuchunguza majina ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, utapeli wa mapenzi, makundi ya ngono kwenye WhatsApp na nyumba zinazotumika kurekodia video za ngono.

Image result for RC Makonda
RC Paul Makonda

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Oktoba 31, 2018 jijini Dar Es Salaam amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na watalaamu wa IT na watu wa Ushauri Nasaha ili watakaobainika kuathirika zaidi waweze kupatiwa ushauri.

Tumefikiria tuunde kamati, kamati itakayokuwa kwenye makundi manne, moja itakayodeal na kundi lote la mashoga, wanaojitangaza na wale wasiojitangaza lakini wanajulikana ni mashoga..Kazi ya Kamati hii ni kushughulika na watu wote wanaoigiza picha za ngono ndani ya mkoa wetu, na nimeshapata taarifa nyumba takriban 24 wanazofanyia kazi, wanachukua wakina dada, wanawanywesha madawa, wanawafanyisha wanachowafanyisha, wanawarekodi, kisha wanawarusha. Pia kuna ambao wanakubali wenyewe, wanalipwa, wanatengeneza picha za ngono, zile picha tunazoona zinazagaa Kariakoo kumbe zingine zinatengenezwa hapa hapa Dar es salaam. ni wale wanaojitangaza kwenye mitandao, na kufanya biashara kwa njia ya mtandao, kwa mfano kuna kundi linaitwa Pachu pachu kuna siri zote za video za ngono.“amesema RC Makonda.

Kwa upande mwingine, RC Makonda amesema kuwa wote watakao tuhumiwa kwa ushoga watapimwa ili kupata uthibitisho.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents