Burudani ya Michezo Live

RC Makonda awachana Watanzania kupitia Ommy Dimpoz ‘tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji’

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amekerwa na baadhi ya tabia za Watanzania za kupenda kutangaza habari mbaya tu za vifo na sio zile nzuri kwa kudai kuwa huo ni unafiki.

RC Makonda na Ommy Dimpoz

RC Makonda akimtolea mfano msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz, amesema kuwa kuna watu kipindi msanii huyo anaugua, walikuwa wanatangaza amefariki dunia, leo amepona na ametoa wimbo wake mpya wa kumshukuru Mungu watu hao wamekaa kimya kama hawajui.

Ukitaka kujua watu walivyo wa Ajabu tazama leo, Ommy dimpo alikuwa mgonjwa sana na ikafika hatua ya watu kutangaza Amekufa. Leo amerejea tena akiwa na wimbo wa kumshukuru Mungu wamekaa kimya Kama vile siyo wao waliokuwa wana post kumwombea apone. Angefariki tungeona mitandao yote imechafuka RIP Ommy oooh umeenda bado tunakuhitaji. Unafiki huu sijuwi utaisha lini, tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji,“ameandika RC Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ommy Dimpoz kwa sasa amerejea nchini akitokea Ujerumani alikokuwa akitibiwa kwa takribani miezi miwili.

Tangu aanze kuugua Ommy Dimpoz, RC Makonda amekuwa ni mtu wa karibu kumjulia hali, na kuna kipindi alishawahi kuujulisha umma juu ya afya ya Ommy.

Image result for RC MAKONDA VS OMMY DIMPOZ

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW