Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

RC Makonda awapa miezi 4 wafanyabiasha wa soko la Urafiki

By  | 

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,Paul Makonda amewapa muda wa miezi 4 wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko Urafiki linalojulikana kama Mahakama ya Ndizi kuhama katika eneo hilo kutekeleza agizo la Mahakama kwa kuwa eneo hilo ni mali ya kiwanda cha urafiki.

Makonda amesema hayo Jumatano hii na kudai kuwa wafanyabiashara hao hawawezi kuhamishwa kama ilivyokuwa awali bali wanatakiwa kuhama baada ya miezi minee kupita na kusema wakati huo Serikali itakuwa imeshawaandalia eneo maalum la kwenda ili kuepukana na matatizo kama hayo tena. 

“Mtafanya biashara kwenye hili eneo kwa muda wa miezi minne hamtaondolewa leo wala kesho kama ilivyokuwa imepangwa bali tumeongeza siku 120 lakini pia nimemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo tayari kuna eneo limepatikana, tunataka tukamilishe utaratibu wa uhalali wa lile eneo ili watu wakienda pale wasipate matatizo kama haya yanayojitokeza ya kufukuzana fukuzana”¬†alisisitiza Makonda

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa katika eneo ambalo watapewa litakuwa limeboreshwa zaidi ili wafanyabiashara hao waweze kupata wateja wa kila aina kwa kudai kuwa walipo sasa wanawakosa baadhi ya wateja kutokana na miundombinu ya soko hilo kutokuwa rafiki kwa baadhi ya watu.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW