Tupo Nawe

RC Makonda awatuliza mashabiki wa Simba baada ya kauli ya Mo Dewji, Kigwangala ahoji juu ya hili

RC Makonda awatuliza mashabiki wa Simba baada ya kauli ya Mo Dewji, Kigwangala ahoji juu ya hili

Baada ya kupoteza fainali ya #MapinduziCup – Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya #SimbaSC, Mohammed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi yake na kubaki kama Mwekezaji.

Mo ameandika ujumbe wa kujiuzulu Uenyekiti katika bodi ya Simba na badala yake atabakia kama mwekezaji tu, Ameandika ujumbe huo dakika chache tu baada ya @simbasctanzania kupokea kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Mtibwa Sugar na kupelekea kukosa Ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi

Baada ya ujumbe huo mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam RC Makonda amewataka mashabiki wa Simba kuwa wapole kutokana na ujumbe huo wa Mo Dewij.

Ujumbe wa Makonda ni huu “Matokea ya Mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole Kwa team yangu ya Simba pamoja na Mashabiki wote na wanaoitakia mema SIMBA. Sina uhakika na kinachoendelea kwenye Ac ya MO kama ni @moodewji mwenyewe ameandika. Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa Wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga Amani na utulivu wa Team zetu. Simba nguvu moja.”

Huo ndio ujumbe wa Rc Makonda lakini pia Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla hakukaa kimya nae akahoji juu ya hili”

Mbali na hilo Mbunge wa Chalinze ambaye ni mtoto wa rais mstaafu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Ridhiwani Kikwete nae aliamua kutoa ushauri kwa Bwana Mo Dewij na kusema haya:-

Wewe unamaoni gani juu hili linaloendelea sasa hivi, unahisi Mo Dewij akiwa kama muwekezaji wa Simba amefanya maamuzi sahihi ya kuondoka katika Uenyekiti wa Bondo ya Simba na kubakia kama Muwekezaji tu….?

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW