Habari

RC Makonda “Hata inyeshe mvua sitaacha kwenda Wasafi Festival Dar”

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea kumshukuru Rais wa WCB, Diamond Platnumz ambaye wiki hii alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kutoa msaada kwaajili ya watoto wenye matatizo ya moyo.

Muimbaji huyo na team yake, alifanikisha kukusanywa tsh milioni 84 kwaajili ya matibabu ya watoto ambao walikuwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo ambayo ni tsh milioni 2 kwa kila mtoto mmoja.

RC Makonda kupitia mtandao wake wa Instagram amesema atumuunga mkono muimbaji huyo kwa kwenda kwenye tamasha hiyo ambalo linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Posta Kijitonyama.

“Diamond Platnumz umeweka alama kubwa sana moyoni mwangu , hata kama Mvua itanyesha nakuhakikishia nitakuja na kuushuhudia upendo wako kwa watoto wa kitanzania abao umeokoa maisha yako,” aliandika RC Makonda.

RC Makonda amekuwa akiendesha kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kitengo hicho cha moyo kwamba kuna watoto zaidi ya 500 wameshindwa kutibiwa kutokana na gharama hizo za matibabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents