Habari

RC Makonda kula sahani moja na wanaowatumia watoto waishio mazingira magumu kama kitega uchumi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda ametangaza vita na watu wenye tabia za kuwachukuwa watoto yatima,walemavu na waishio katika Maisha magumu Kama mitaji ya kujinufaisha.

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kinyume na Sheria hali inayopelekea kushindwa kutumia fursa ya Elimu Bure iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

Utafiti huo umebaini Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya watoto 3,312 wanafanya kazi mitaani na kati ya hao watoto 2,984 walionekana wakifanya kazi nyakati za mchana na 328 wanafanya kazi nyakati za usiku.

RC Makonda amesema idadi hiyo ya watoto wanaoishi mitaani ni matokeo ya kukosekana kwa misingi bora ya familia na mmonyoko wa maadili ndio maana aliamua kuunda tume ya kupitia sheria ya mtoto na mikataba ya kimataifa ambayo itasaidia kuweka haki stahiki za watoto.

Aidha RC Makonda amewaonya watu wenye tabia ya kuwapatia ombaomba fedha barabarani kuwa Ndio wanaohalalisha uwepo wa watu hao ambapo amesema Kama mtu anataka kweli kusaidia waishio maisha magumu wapeleke misaada kwenye vituo vilivyopo kwa mujibu wa sheria kwakuwa vituo hivyo vinafuatilia mienendo ya watoto kitabia, elimu na matibabu ambapo ukimpa pesa mtoto barabarani unatengeneza mazingira ya kuwa na fedha ambayo hana uhalali nayo na anapokuwa mtu mzima anakuwa mkabaji,mporaji na kuchoma visu watu wasio na hatia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents