Michezo

Real Madrid, Bayern Munich wanahitaji miujiza ya Mungu kutwaa kombe msimu huu

Klabu kubwa mbili barani Ulaya za Real Madrid na Bayern Munich zinahitaji msaada wa Mungu kutwaa kombe lolote barani Ulaya kwenye msimu huu mpya wa 2018-19 .

Image result for bayern munich and real madrid

Hii ni kutokana na matokeo mabovu ambayo klabu hizo zinayapata kwenye ligi zao za ndani yaani La Liga na Bundesliga.

Bayern msimu huu tayari imeshafungwa michezo mitatu na kushinda mechi 6 huku wakipata sare michezi miwili kwenye michezo 11 ya Bundesliga, Performance ambayo ni mbovu zaidi kutokea ndani ya klabu hiyo kwa miaka 15.

Bayern jana walipoteza mchezo muhimu dhidi ya Borussia Dortmund kwa kufungwa goli 3-2 na kuifanya klabu hiyo ishuke hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Bundesliga.

Matokeo ya Bayern kiujumla kwa msimu huu hayaridhishi na yote hayo yanachangiwa na mabadiliko ya benchi la ufundi.

Wakati hayo yakijiri nchini Ujerumani, kule nako Hispania hali ya mabingwa barani Ulaya, Real Madrid nayo sio shwari hii ni kutokana na kuwa na kiwango cha chini kwenye ligi hiyo.

Madrid mpaka sasa wapo nafasi ya 6 katika Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga).  matokeo mabovu ya Madrid yamechangiwa pia na kuhama kwa wachezaji na kocha wao wa zamani Zinedine Zidane.

Bado hata hivyo, klabu zote mbili mwenendo wao kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya sio zuri kama klabu hizo zilivyozoeleka miaka ya nyuma.

Muda bado, lakini kwa msimu huu ni ngumu sana kwa klabu hizo kutwaa kombe kubwa barani Ulaya au hata ndani ya nchi zao hii ni kutokana na mabadiliko na madhaifu wanayoyaonesha kwenye michezo yao.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents