Michezo

Real Madrid na Atletico Madrid marufuku kusajili

Mahasimu soka wa Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid wamepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya sokoni kwa vipindi viwili.

160114125839_real_madrid_atletico_champions_league_512x288_getty

Klabu hizo mbili zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani Fifa baada ya kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusu kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto.

Lakini marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kununua wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.

Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents