Michezo

Real Madrid na Barcelona zaipiku Manchester United kwenye nafasi ya kwanza ya vilabu tajiri zaidi duniani

Real Madrid imetajwa kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa kampuni ya uhasibu ya Deloitte. Kabu hiyo ya Uhispania inathamani ya pauni milioni 674.6

Man Utd imeshuka hadi nafasi ya tatu baada ya Barcelona ambayo ni klabu nyingine kutoka Uhispania kuchukua nafasi ya pili, ilisema.

Kulikua na jumla ya vilabu sita vya Ligi ya Uingereza vilivyojumuishwa katika orodha ya vilabu kumi tajiri zaidi duniani.

Orodha ya vilabu tajiri zaidi duniani ambayo huchapishwa kila mwaka na kampuni ya Deloitte hunaangazia thamani ya vilabu bila kujumuisha madeni.

Real Madrid ilishinda taji la ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuinyuka Liverpool mabao 3-1 mjini Kiev mwezi Mei mwaka uliopita.


Mapato ya Real Madrid yaliongozeka baada ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa mara tatu mfululizo

Ushindi huo uliisadia Real kuongeza mapato yake na kuifanya kuwa timu yenye mapato makubwa mara kumi na mbili katika orodha ya Deloitte

Klabu hiyo ilishuhudia ukuaji wa biashara yake kwa pauni milioni 54.8, iliyojumuisha ongezeko la wadhamini,mapato ya uuzaji wa bidhaa zao na kuongezeka kwa ziara ya kabla mwanzo wa msimu.

Real Madrid imevuja rekodi kwa kukusanya mapato ya kibiashara ya jumla ya pauni milioni 356.2 kiwango ambacho kimeifanya kuwa klabu tajiri zaidi duniani ukilinganisha na vilavu vingine.

Dan Jones, mkuu wa kitengo cha uhasibu wa masuala ya michezo katika kampuni ya Deloitte, amesema: “matokeo bora ya Real Madrid mwaka 2017-18 yamechangia historia ya ufanisi wao uwanjani ikiwa ni pamoja na ushindi wa hivi karibuni wa mataji matatu ya ligi ya mabingwa.

Hii imeiwezesha klabu kupata matangazo ya biashara kwa sababu makampuni yapendelea sana kushirikiana na vilabu vilivyo na ufanisi mkubwa barani Ulaya.”

Amesema nyingi ya vilabu kumi bora kwenye orodha ya Deloitte huwa ni vile vilivyofuzu kufika hatua ya 16 bora katika mchuano wa ligi ya mabigwa kwa sababu vina nafasi ya kukua kibiashara.

Vilabu vya Bayern Munich na Manchester City vilisalia katika nafasi zao kwa miaka miwili iliyopita.

Paris St-Germain, Liverpool, Chelsea, Arsenal, na Tottenham Hotspur walishikilia nafasi ya sita hadi kumi.

Everton walishikilia nafasi ya 17, Newcastle United ya 19, na West Ham United nafasi ya 20.

Vilabu vyote 20 vilivyo kwenye nasi ya ”tano bora” vinashiriki ligi kuu za mataifa ya bara ulaya, ikiwa ni pamoja na Italia iliyonyakua nafasi nne, nazo Ujerumani na Uhispania zikichangiavilabu tatu, huku Ufaransa ikisalia na nafasi moja.

Matokeo mengine yanajumuisha:

  • Spurs wamepewa nafasi ya kucheza msimu kamili katika uwanja wa Wembley ambao umeona ongezeko la mapato ya siku ya siku kwa 54%
  • Mapato ya Paris Saint-Germain yameshuka kwa miaka miwili mtawalia
  • AS Roma na AC Milan wamerejea katika orodha ya 20 bora baada ya kuandikisha matokeo bora katika mashingano ya Uefa
  • Mabingwa wa Uturuku Besiktas wamepata ufanisi mkubwa baada ya kuorodheshwa nambari 26.

“Uwepo mkubwa wa vilabu vya ligi ya Uingereza unaendelea kushuhudiwa katika orodha Deloitte ya kila mwaka ya vilabu tajiri duniani”,alisema Sam Boor.

Chanzo https://www.bbc.com/swahili/michezo-46985532

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents