Burudani

Real Madrid walimtaka Mourinho akawatosa

Imedaiwa kuwa Read Madrid walimpa ofa Jose Mourinho ili arejee tena Santiago Bernabeu.

José Mourinho

Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon ameiambia Sky Sports kuwa rais wa sasa Florentino Perez alimtaka Mourinho arejee kwenye klabu hiyo kabla ya kuamua kumpa Zinedine Zidane baada ya kumtimua Rafael Benitez.

“Nadhani sio siri kuwa rais wa sasa alimpenda sana Jose Mourinho na Perez aliwasiliana naye kabla ya kuamua kumchukua Zidane,” alisema Calderon.

“Inavyoonekana, Mourinho hakupenda kuja kipindi hiki cha msimu na Zidane alikuwa hapa kwahiyo itabidi tusubiri kuona nini kitatokea wiki chache zijazo.”

Manchester United pia wamedaiwa kuwa na nia ya kumchukua kocha huyo aliyetimuliwa na Chelsea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents