Michezo

Real Madrid waondolewa mashindano ya ‘Copa Del Rey’ kwa kumchezesha mchezaji Denis Cheryshev

Klabu ya Real Madrid imeondolewa katika michuano ya Copa del Rey kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakufaa kuchezeshwa wakati wa mechi yao dhidi ya Cadiz Jumatano.

deni

Mchezaji huyo, Denis Cheryshev, ndiye aliye funga goli la kwanza katika mechi ya Real ilishinda 3-1.

Winga huyo wa Urusi alifaa kuwa akitumikia marufuku, aliyopewa alipokuwa Villarreal kwa mkopo.

Lakini yeye na klabu yake ya Real, wanasema hawakujuzwa hilo kabla ya mechi hiyo.

Klabu hiyo imesema itachukua “hatua ifaayo” kuhakikisha matokeo “ya kuridhisha”. Cheryshev, 24, aliondolewa uwanjani muda mfupi baada ya mapumziko, baada ya Real kugundua kosa hilo.

Real wameshinda kombe hilo mara 19, majuzi zaidi ikiwa 2014.

Jaji wa Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) Rubio Sanchez alisema ushindi wa mechi hiyo sasa utakabidhiwa Cadiz.

Real pia wametakiwa kulipa faini ya euro 6,001 (£4,300).

Gazeti la Uhispania la Marca limeripoti kuwa Real watakata rufaa uamuzi huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents