Michezo

Real Madrid wapanga kumsajili Pogba baada ya msimu huu

Real Madrid walishindwa kunasa saini ya Paul Pogba alipoamua kurudi Manchester United kwa dau la pauni milioni 89 mwaka 2016.

Paul Pogba kwa sasa ni miongioni wachezaji wanaowindwa na timu ya Real Madrid kutokana na taarifa zilizotolewa na The Sun mabosi wa Bernabeu sasa wanapanga jitihada za kumsajili Pogba wakati msimu huu utakapomalizika.

Real wanafuatilia hali ya mchezaji huyo huko Manchester United baada ya kiungo huyo kushindwa kumridhisha meneja Jose Mourinho hivi karibuni baada ya kushuka kifomu.

Paul Pogba mwenye umri wa miaka 24 ndiyo kwanza anatumikia mwaka wake wa pili kati ya mitano aliyosaini hapo awali na United. Inafahamika kwamba kwa sasa timu hiyo haipo tayari kumuachia kiungo huyo lakini itategemea maamuzi ya mchezaji huyo ambaye wakati mwingine anaonekana kutokwa na furaha katika msimu huu.

Na kama msimamo huo ulibadilika Old Trafford Wahispania hao watahitaji kutoa zaidi ya Pauni milioni 120 ili kummpata mchezaji huyo ambaye hapo awali alishawahi kuwa mchezaji ghali duniani.

Pogba alifanyinywa mabadilisho katika mechi dhidi ya Tottenham mwezi uliopita na kutokea benchi katika mechi dhidi ya Huddersfield na pia alitolewa katika mechi dhidi ya Newcastle.

Mourinho amekuwa akimuunga mkono nyota yake kwa kumsifia kiwango chake tangu alipo rudi Old Trafford.

Pogba alishinda mataji mawili katika msimu wake wa kwanza huko United baada ya kuondoka Juventus. Kwa sasa kiungo huyo hana nia ya kuondoka United.

Lakini hilo haliwafinyi Real Madrid kuacha kujaribu kumbadili mawazo yake ikiwa vitu vitamuendea vibaya zaidi kabla ya msimu huu kuisha.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents