Uncategorized
Real Madrid watawazwa kuwa mabingwa wa klabu bingwa wa Dunia
Real Madrid imetawazwa kuwa mabingwa wa klabu bingwa duniani baada ya kuwafunga timu ya Al Ain kwa jumla ya mabao 4-1 kwenye mchezo wa hatua ya fainali iliyopigwa siku ya Jumamosi usiku.
Mabingwa hao wa klabu bingwa barani Ulaya wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo wakatimabao yao yakiwekwa kimyani na Modric 14’ Llorente 60’Ramos 78’ Nader 90’+1 (OG) (Shiotani 86’).