Michezo

Real Madrid yawanyapia Neymar na Kylian Mbappe, wakati PSG ikichunguzwa na UEFA

Klabu ya Real Madrid ipotayari kuipatia Paris Saint-Germain kitita kinono cha fedha endapo italazimika kuwauza wachezaji wake Neymar au Kylian Mbappe ili kuepuka sheria za Chama cha soka barani Ulaya dhidi ya udhibiti wa fedha (FFP).

UEFA ilianzisha sheria ya fedha ili kudhibiti klabu kutofanya matumizi makubwa zaidi kuliko kile wanachokiingiza hali ambayo itapelekea kutumbukia kwenye janga la kiuchumi.

Kitendo cha klabu ya PSG kufanya usajili mkubwa kwa wachezaji wake wawili, Neymar iliyowagharimu pauni milioni 200 na Mbappe pauni milioni 166 kinawaweka chini ya uchunguzi wa UEFA kupitia sheria hiyo ya fedha.

Kwa mujibu wa gazeti la Hispania AS, mabingwa hao wa klabu bingwa barani Ulaya Real ni muda mrefu imekuwa ikiwatamani Neymar na Mbappe hivyo hali hiyo inawafanya kuwamakini na tayari kwa lolote endapo PSG ilatalazimika kumuuza mmoja wapo.

Iicha ya kuripotiwa kuwa PSG inachunguzwa dhidi ya sheria hiyo ya fedha ya FFP, lakini klabu hiyo inaendelea nampango wake wa kuhakikisha inawalinda wachezaji wake na kuendelea kuwa nao kwa kadri iwezekanavyo.

Wenyewe Real wamekuwa wakisaka saini ya nyota hawa kwa hudi na uvumba baada ya kumuuza staa wao Cristiano Ronaldo kwenda Juventus.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents